Katika mabaraza ya mipango ya Khatami, muda mrefu sasa imethibitishwa kamba lazima zichukuliwe hatua nyingi ili kufungua nafasi mpya za kazi. Nafasi laki nane kwa mwaka -hilo lilikuwa lengo fahari la mpango wa wakati huu wa miaka mitano - lakini labda robo tu ya jumla hiyo itaweza kufikiwa. Sababu kubwa hapa ni kukosekana rasmilmali za kutosha kutoka nchi za nje. Waziri wa uchumi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Werner Müller anaizuru Iran mwishoni mwa wiki hii, na hii leo mjini Teheran atatia saini mkataba wa vitega uchumi na kinga, ambao unatarajiwa kuwa shina la juhudi kubwa za uchumi wa Ujerumani nchini Iran. Na kuna uhusiano wa pembezoni tu katika kampeni ya uchaguzi mkuu hapa Ujerumani, Müller aliposema kabla ya safari yake, kwamba kile kinachohusika hasa ni kujipatia nafasi bora uchumi wa Ujerumani. Hii inamaanisha pia kupunguza jumla ya watu waisokuwa na kazi hapa nchini. Makampuni ya Ujerumani yamekuwa yakiwakilishwa muda mrefu sasa nchini Iran -katika seka ya mafuta ya ardhini, tawi la magari, mawasiliano sawa na chumapua, tumbaku na uchimbaji madini. Na ingawa katika baadhi ya sekta hizi yamepatikana maendeleo zaidi mnamo miaka michache iliyopita, hatahivyo wajuzi wa hali ya mambo wakadiria kwamba kuna nafasi zaidi ya kuimarika. Ingawa Iran inakabiliwa na hali ya kuzorota uchumi, jambo ambalo limesababishwa na vita vya miaka minane pamoja na Iraq, kuanguka bei ya mfuta na madeni makubwa ya taifa, hatahivyo Iran imefanikiwa kuendelea kulipa madeni yake na sasa ni chini ya Dola bilioni saba.
http://www.iuni.com/...tware/web/index.html
Links Plugins
http://www.iuni.com/...tware/web/index.html
Links Plugins